Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Mji wa Masasi

 Moja ya Bustani ya Mfano maonesho ya Nane Nane 2016 Ngongo Manispaa ya Lindi. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi.Gimbana Ntavyo(kulia) akiwa kwenye Viwanja Vya Nane Nane Ngongo. Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akizungumza na mmoja wa wajasiliamali kwenye maoensho ya Nane Nane. Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh: Godfrey Zambi akikagua Bidhaa ndani ya Banda la Halmashauri ya Mji Masasi Afisa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Masasi Rehema Charles akionesha utaalamu wa utengenezaji wa Chakula cha mifugo. Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni Banda la Magereza. Waziri wa Nishati na Madini Prof; Sospeter Muongo akikagua baadhi ya Mabanda ya Maonesho.

Karibu kwenye Tovuti ya Halmashauri ya Mji wa Masasi

Halmashauri ya mji wa masasi ni miongoni mwa Halmashauri nane zinazounda mkoa wa mtwara na inatawaliwa na jimbo moja la Masasi ambapo Halmashauri ya mji ina jumla ya kata 14,tarafa 2,mitaa 58, vijiji 31 na vitongoji ni 150. Halmashauri ya mji Masasi ilianzishwa julai mwaka 2012, Halmashauri ya mji Masasi ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 400.Halmashauri hii ilizaliwa kutokana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, ambayo kabla ya kuwa Halmash...

Takwimu

 • Kata = 14
 • Shule za Msingi = 35
 • Shule za Sekondari = 10
 • vijiji = 31
 • Zahanati = 11
 • Ukubwa wa Eneo kilometa za Mraba = 400
 • Idadi ya Watu = 102,696

Habari & Matukio

10 Aug 2016

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.

09 Aug 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hasani amepiga marufuku uchomaji moto wa misitu katika mikoa ya Lindi na Mtwara lengo likiwa ni utunzaji wa mazingira.