Halmashauri ya mji wa masasi ni miongoni mwa Halmashauri nane zinazounda mkoa wa mtwara na inatawaliwa na jimbo moja la Masasi ambapo Halmashauri ya mji ina jumla ya kata 14,tarafa 2,mitaa 58, vijiji 31 na vitongoji ni 150. Halmashauri ya mji Masasi ilianzishwa julai mwaka 2012, Halmashauri ya mji Masasi ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 400.Halmashauri hii ilizaliwa kutokana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, ambayo kabla ya kuwa Halmashauri ya Mji, kama ilivyo matakwa ya kisheria, ilipitia hatua za takribani mwaka mmoja kuwa na hadhi ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Masasi. Sheria iliyounda na inayoongoza utendaji wa Halmashauri hii ni Sheria ya Halmashauri za Mitaa (Mamlaka za Mji), Sura ya 288, ya mwaka 2002. Idadi ya wakazi Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 102,696 kati yao wanaume ni 49,111 na wanawake ni 53,585 ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa mji wa masasi wanategemea shughuli za kilimo kwa ajili ya kujipatia chakula na kipato ambapo wengine hujishughulisha na shughuli mbalimbali kama biashara na ajira katika sekta ya umma. Utawala Halmashauri ya mji wa masasi ni miongoni mwa Halmashauri saba zinazounda mkoa wa mtwara na inatawaliwa na majimbo mawili ya Lulindi pamoja na masasi mjini ambapo Halmashauri ya mji ina jumla ya kata 14,tarafa 2,mitaa 59, vijiji 30 na vitongoji ni 143. Shughuli za kiuchumi Shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Halmashauri ya mji wa masasi zimegawanyika katika Nyanja mbalimbali ikiwemo biashara na kilimo ambapo mazao makuu ya biashara ni pamoja na ufuta, karanga, choroko, korosho, njugumawe na mbaazi ambapo kwa upande wa mazao ya chakula ni mahindi, mtama, mpungapamoja na mihogo.Kwa ujumla Mkulima wa Masasi mjini ni mkulima mdogo anayetumia jembe la mkono na ambaye anapata tija ndogo kutokana na uwekezaji anaoufanya katika ardhi, nguvukazi na fedha.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.