Idara ya Kilimo ya Halmashauri ya Mji inatoa huduma zifuatazo kwa wanainchi wa eneo la Halmashauri ya Mji masasi. Huduma hizo ni:
Idara inatoa ushauri wa kanuni za Kilimo bora cha Mazao yote yanayolimwa kwenye ukanda huu.
Kuleta na Kufundisha Teknolojia mpya zinazoletwa na kugunduliwa na vituo vya utafiti wa Kilimo.
idara pia ina ratibu na kusimamia upatikanaji wa Hali ya chakula katika maeneo yanayolima na yale yanayotegemea kununua chakula toka maduka ya wafanyabiashara.
Inaandaa vipindi na kushirikiana na wadau mbalimbali wenye vyombo vya habari ili kuweza kuhakikisha elimu inawafikia wakulima wengi kwa wakati mmoja.
Inaandaa na kugawa miche ya mikorosho kwa wakulima ili kuhakikisha uchumi wa wakulima unaimarika.
idara ya Kilimo pia inaandaa njia mbalimbali/mbinu za kufikisha ujumbe/elimu kwa wakulima kwa njia ya Mashamba darasa, Maonyesho mbalimbali yakiwemo ya Nanenane.