• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

HALMASHAURI YA MJI MASASI YANG’ARA KITAIFA KWENYE MASHINDANO YA STADI ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA SAYANSI KWA SHULE ZA MSINGI.

Posted on: June 14th, 2025

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (MB), amemkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni Mbili na Laki Tano pamoja na cheti cha pongezi Mwalimu Haji Mohamedi Ligalawa wa  Shule ya Msingi Mtandi iliyopo Halmashauri ya Mji Masasi kwa kuibuka mshindi wa tatu kati ya washiriki 148 katika Shindano la Stadi za Ufundishaji wa Masomo ya Sayansi kwa shule za Msingi. 

Zawadi hiyo imetolewa Juni 14, 2025, katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waheshimiwa Wabunge, na viongozi wa Taasisi mbalimbali.

Akiongea baada ya Hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji Masasi, Kaimu Afisa Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Mji Masasi Mwl. Joseph Amlima, ameipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania kwa Kuandaa Mashindano hayo ambayo huwafanya Walimu kuwa bora zaidi. 

Aidha amempongeza Mwl. Haji Ligalawa kwa ushindi huo mkubwa kwa kubainisha kuwa ameiheshimisha Halmashauri ya Mji Masasi na Mkoa wa Mtwara kwa Ujumla wake huku akitoa wito kwa Walimu wote wa Mji Masasi kuendelea kujitokeza kwenye Mashindano hayo ili waweze kuonesha umahiri wao katika ufundishaji na ubunifu unaozingatia Mtaala Mpya wa Elimu.

Shindano hilo huandaliwa kila mwaka na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi BOOST. 

Kwenye picha upande wa kulia aliyevaa miwani ni Kaimu Afisa Elimu ya Awali na Msingi Halmshauri ya Mji Masasi Mwl. Joseph Amlima, Waziri wa elimu (katikati)  na mshindi mwalimu Haji.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • DC MASASI MHE. KASSANDA AKABIDHI ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOMAINDO, ASEMA DKT SAMIA AMEWAPA TABASAMU KUPITIA “SAMIA BONANZA MASASI”

    June 15, 2025
  • HALMASHAURI YA MJI MASASI YANG’ARA KITAIFA KWENYE MASHINDANO YA STADI ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA SAYANSI KWA SHULE ZA MSINGI.

    June 14, 2025
  • RC MTWARA ARIDHISHWA NA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI MATAWALE, AWAHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII

    June 11, 2025
  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.