• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

Idara ya Fedha

Idara ya Fedha

Idara ya fedha ni idara inayojishughulisha na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha katika halmashauri na kutoa ushauri wa namna bora ya matumizi ya fedha.

Majukumu  ya idara hii ni:

  • kusimamia na  kuhakikisha kunakuwa na mfumo thabiti wa udhibiti wa ndani (lnternal control system) Ambao pamoja na kuzingatia masuala ya kiutendaji pia unalenga katika kuangazia taratibu nzima za kifedha za halmashauri.
  • Idara hii ina kazi ya kuwasilisha taarifa  za kifedha kwenye kamati ya fedha na utawala kwa ajili ya mapitio,pia kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha wa matumizi bora ya mali za halmashauri   ikiwa ni pamoja  na mpango kazi mzuri wa wafanyakazi na utawala ndani ya idara zote za  halmashauri katika masuala yote yanayohusuyo mambo ya fedha.


Idara ya fedha ina jumla ya vitengo 4, Ambavyo ni:

  • Kitengo cha mishahara,
  • kitengo cha mapato,
  • kitengo cha matumizi,
  • kitengo  cha kufunga  mahesabu  (Final account),

 Kazi za vitengo hivyo ni kama ifuatavyo;

  • MATUMIZI
  • Kuandaa malipo yote
  • Kuandaa Bajeti ya matumizi ya kawaida,
  • Kuhakikisha uwepo wa nyaraka zote za malipo kabla na   baada ya kulipa,
  • Kuhakikisha taratibu na sheria za kifedha zinatekelezwa,
  • kuhakikisha kuwepo na majalada ya kumbukumbu kwa malipo yaliyolipwa,
  • Kufanya usaili wa kimahesabu kati ya benki na vitabu vya kumbukumbu vya halmashauri.
  • Kuandaa taarifa za fedha na kuziwasilisha sehemu husika kwa wakati.

2: MAPATO

  • Kuhakikisha inakusanya mapato yote ya halmashauri,
  • Kuhakikisha kuna udhibiti mzuri wa mapato ya Halmashauri,
  • Kupeleka fedha taslimu na hundi benki
  • Kuandaa ripoti mbalimbali na kuziwasilisha sehemu husika,
  • Kuweka utaratibu rahisi wa malipo ya fedha taslimu kwa wateja.
  • Kubuni vyanzo vipya vya mapato,

3: MlSHAHARA

  • Kuandaa orodha ya watumishi kwa ajili ya kulipwa mishahara
  • Kutunza orodha ya watumishi wanaolipwa mishahara na kutunza kumbukumbu za makato yakatwayo watumishi kwenye mishahara yao
  • Kuandaa bajeti ya mishahara kwa watumishi
  • Kuandaa taarifa mbalimbali za mishahara na kupeleka sehemu husika
  • Kushughulikia matatizo yote ya mishahara inayotokea kwa watumishi.

4: KITENGO CHA TAARIFA ZA KIMAHESABU (Final account)

  • Kuandaa usuluhisho wa taarifa za cashbook zinatunzwa halmashauri na zile zilizopo benki
  • Kujibu hoja za ukaguzi
  • Kuanda taarifa za mapato na matumizi
  • Kutunza cashbook.

Katika kufanikisha shughuli za idara mifumo mbali mbali hutumika katika kazi hizi, baadhi ya mifumo inayotumiwa idara hii ni:

  • EPICOR
  • LGRCIS
  • FFARS

KITENGO CHA BIASHARA

Kitengo cha biashara kina watumishi wawili kwa sasa, na kitengo hiki kiko chini ya idara ya fedha.

  • Masoud Mwinjuma  mkuu wa kitengo – 0786771811
  • Sheha J. Satmah                                    _0685352522

Kitengo hiki kina majukumu yafuattayo:

  • Utoaji wa leseni za Biashara kwa wafanya biashara wote wanaotoa huduma ndani ya eneo la halmashauri ya mji kwa mujibu wa Sheria za Leseni za Biashara na 25 ya 1972 pamoja na marekebisho yake.
  • Utoaji wa leseni za vileo kwa mujibu wa sharia za Vileo namba 28 ya 1968 na marekebisho yake.
  • Usimamizi na Ukusanyaji wa Ushuru wa Huduma “Guest House Levy) kwa Mujibu wa sheria ya fedha namba 16 ya 2015 sura 290.
  • Kukusanya Takwimu za wafanyabiashara na Masoko waliopo eneo la Halmashuri ya Mji.

UTARATIBU WA KUPATA LESENI.

  • Mfanya biashara anapaswa kuwa na Tin namba ambayo inapatikana pfisi za Mamlaka ya Mapato (TRA)
  • Atapewa fomu ya maombi ya Leseni ambayo anapaswa kuipitisha kwa maafisa wafuatao:
  • Afsa Mtendaji wa Eneo Husika
  • Afsa Afya
  • Afsa Mipango Miji
  • Baada ya ukaguzi ataandaliwa ankra ya malipo (bili) ambapo atapaswa kwenda kulipia Benki au kwa Wakala wa Benki Husika.
  • Baada ya Malipo atapatiwa Leseni anayohitaji na risit ya malipo.

Ikumbukwe kuwa kila Biashara inabei yake hii ni kwa Mujibu wa Sheria ya Leseni ya Biashara NA 25 ya 1972.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • .STANDI YA MAEGESHO YALETA FURSA KWA WANANCHI MASASI.

    March 22, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.