Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Rachel Kassanda amewahimiza wananchi wa Masasi kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kibingwa za uchunguzi, vipimo na matibabu ya saratani bure kuanzia tarehe 22 April 2025 hadi 25 April 2025 zinazotolewa na Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Masasi Mji katika Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara ( Huduma za Mkoba-Samia Suluhu Outreach Services).
Amesema hayo April 23, 2025 mara baada ya kuwapokea madaktari bingwa kutoka taasisi ya Ocean Road ambao wameanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa huduma za kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Crispin Kahesa amesema huduma zinazotolewa ni vipimo na matibabu ya saratani bure (saratani ya matiti na mlango wa kizazi, vipimo na matibabu ya tezi dume bure kutoka kwa madaktari bingwa.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkomaindo, Dkt. Ditrick Mmole amesema wananchi wengi wamejitokeza kupata huduma hizo na wanatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya 1000.
Mwananchi kutokea Mkuti, Hawa Ally Mohamed amesema amepata mapokezi mazuri na tiba bila gharama yeyote huku akiwahimiza wakazi wa Masasi na maeneo mengine kufika kupata huduma hizo za matibabu ambazo zinatolewa bure kabisa.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.