Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala amekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa shule mpya ya sekondari ya Matawale uliogharimu zaidi ya Tsh milioni 560 ambapo amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na nidhamu ili waweze kufaulu na kusaidia familia na jamii.
Akizungumza na wanafunzi wa shule mpya ya sekondari Matawale leo Juni 11, 2025 katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha katika ujenzi wa shule za sekondari ikiwemo Matawale ili kusaidia wanafunzi kuacha kutembea umbali mrefu hivyo ni wajibu wao kusoma kwa bidii na kufaulu.
Miradi iliyokaguliwa ni miradi ya sekta ya elimu ambapo amekagua shule mpya ya Sekondari Matawale iliyogharimu kiasi cha zaidi ya Tsh Milioni 560 na Shule ya Amali Marika iliyogharimu kiasi cha Tsh bilioni 1.6 ambapo amehimiza kasi zaidi ya utekelezaji wa mradi huo.
Viongozi mbalimbali wameambatana katika ziara hiyo ikiwemo Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Rachel Kassanda, Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na Wananchi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.