UJENZI
UTANGULIZI
Idara ya Ujenzi ni mojawapo ya idara katika Halmashauri ya Mji MASASI, inayofanya kazi kwa
mujibu wa sheria ya uanzishwaji wa serikali za mitaa.
Idara ya Ujenzi imegawanyika katika sehemu tatu,
1.Sehemu ya Barabara
2.Sehemu ya Majengo
3.Sehemu ya Mitambo na Umeme
MAJUKUMU YA IDARA
1.Kusimamia ujenzi na Ukarabati wa majengo yote ya Halmashauri ya Mji wa masasi.
2.Kusimamia matengezo ya magari ya Halmashauri ya Mji wa masasi.
3.Kufanya tathimini ya miundombinu ya barabara za Mji wa Korogwe na kufanya makadirio ya
gharama za matengenezo
4.Kusimamia wakandarasi wote wanaofanya kazi za ujenzi katika miradi ya Halmashauri.
KUBORESHA BARABARA
•Kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuweza kuboresha barabara za mji kwani kwa sasa
Halmashauri inategemea vyanzo viwili tu ambavyo ni makusanyo ya ndani na Mfuko wa
Barabara.
•Kuelimisha jamii umuhimu wa kushiriki kulinda miundombinu ya barabara.
•Kuelimisha Jamii kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi ya barabara.
•Kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waache kutupa takataka ngumu kwenye mifereji ya maji
ya mvua.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.