Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Prosper Luambano amesema lengo la ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ni kuhakikisha takwimu na nyaraka za utekelezaji wa miradi hiyo zinahifadhiwa na kuandaliwa kwa usahihi, ubora na wakati ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akiambatana na watalaamu wa Mipango na uratibu amesema Ufutualiaji wa miradi ya maendeleo na usahihi wa nyaraka ni miongoni mwa majukumu muhimu ya Divisheni ya mipango na uratibu.
Amesema hayo leo, April 25, 2024 wakati wa ufuatiliaji na utembeleaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo halmashauri ya Mji Masasi.
Miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyofanyiwa ufuatiliaji ni ujenzi wa bwalo na madarasa shule ya sekondari ya kutwa Mwengemtapika, ujenzi ya matundu cha choo shule ya msingi Mwengemtapika na ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo shule ya msingi Mkomaindo.
Ufuatiliaji wa mara kwa mara husaidia kuweka sawa kumbukumbu za utekelezaji, uandaaji wa nyaraka, usahihi wa nyaraka na hatimaye kuleta thamani ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kuu na Halmashauri kupitia mapato ya ndani kwa ustawi wa wananchi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.