• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

ZAWADI NA VYETI VYA PONGEZI KUTOLEWA IKIWA NI JITIHADA ZA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO H/MJI MASASI. KITUO CHA AFYA MBONDE CHAPATA PONGEZI

Posted on: April 9th, 2024

Halmashauri ya Mji Masasi kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imeanzisha utaratibu wa kuwatambua watumishi wa afya na vituo vya kutolea huduma za afya kwa kutoa zawadi na vyeti vya pongezi ikiwa ni mpango mkakati wa  kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kutokomeza vifo vya mama na watoto wachanga.

Zawadi hizo zimetolewa April 9, 2024 katika kikao cha tathmini ya Januari- Machi 2024 cha afya ya uzazi wa mama na mtoto kilichofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Kaimu Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Andrea Kalinga amesema mpango huo ni bora na muhimu katika kutokomeza vifo vya mama na mtoto huku akisisitiza  kuhakikisha mikakati mbalimbali inasimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi.

Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji Masasi, Dkt. Salum Gembe amesema utaratibu wa kuwatambua na kuwapongeza umeanzishwa rasmi kupitia mawazo bora ya timu ya usimamizi wa huduma za afya (CHMT) ili kuongeza ufanisi wa utoaj huduma, ili kutokomeza vifo vya mama na watoto.

" Watumishi hawa wanajitoa sana, wanafanya kazi masaa 24, wakati mwingine wanaingia kwenye shida za kitaaluma au kiutumishi, kwasababu wamebeba jukumu la kuokoa afya za watu.Tumeanzisha utaratibu wa kuwatambua kwa kuwapongeza kwa barua na vyeti, wote wanafanya kazi vizuri lakini leo tutapata ambao watatuwakilisha na hili zoezi litakuwa endelevu "amesema.

Katika zawadi hizo, kituo cha afya Mbonde kimepata cheti kwa kutopata kifo cha mama na watoto wachanga kwa kipindi cha Januari- Machi 2024 na watalamu wa afya waliopata barua za pongezi, Dr. Hashimu chiwaya( Mkomaindo Hospital) Hassani chande(Zahanati ya mumbaka) Atika mussa (Mkomaindo hospitali) na  Edina mkwango (Mkomaindo hospitali)

Aidha, Dkt. Gembe amesema mbali na jitihada hizo mikakati mbalimbali imewekwa ikiwa ni kuimarisha mifumo ya utoaji wa taarifa za akina mama wote wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma, kuimarisha mfumo wa usafirishaji, kukusanya damu salama,  na kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza uwajibikaji miongoni mwa watoa huduma.

Matukio mbalimbali katika picha.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.