Kamati ya Fedha na Utawala ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba April 17, 2024 imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo imekagua jumla ya miradi mitano.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na shule ya sekondari ya kutwa ya Jida, kikundi cha vijana (Wapambanaji) kilichopo kata ya Mkuti, zahanati ya Napupa, shule ya Msingi Nyasa na jengo la upasuaji Mkomaindo.
Akizungumza katika ukaguzi huo, Mhe. Namtumba amesema ushirikiano baina ya waheshimiwa Madiwani na watalaamu ni muhimu katika kuhakikisha Mji unakuwa na maendeleo.
Aidha, Kamati hiyo imepongeza juhudi za Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada zake za kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi wa Masasi Mji sambamba na kutoa shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Pia, Mhe Namtumba amewashukuru marafiki wa Ujerumani (Enzkreis) kwa kuleta vifaa vya Upasuaji katika Jengo la Upasuaji Mkomaindo ambalo limetumia mapato ya ndani kwani vinakwenda kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Sambamba na hilo Kamati hiyo imewapongeza Wahe. Madiwani wote, Mkurugenzi wa Mji kwa kufanikisha kukamilika kwa majengo ikiwemo jengo la Upasuaji Mkomaindo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.