Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Bi. Fatima Kubenea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi ameongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya msingi Darajani iliyopo kata ya Mkomaindo Halmashauri ya Mji Masasi ikiwa ni katika kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi hilo limefanyika April 21, 2024 akiwa ameambatana na Mganga Mkuu wa Mji Masasi Dkt. Salum Gembe akimwakilisha Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, wanafunzi, Mwenyekiti wa kijiji, wananchi na wataalamu mbalimbali.
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yatahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala, usafi na shughuli mbalimbali hadi siku ya kilele cha Siku ya muungano April 26, 2024.
Kaulimbiu “Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa Letu’’.
Matukio katika picha.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.