Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali akikagua bidhaa za Wajasiriamali.
Halmashauri ya Mji wa Masasi imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi 79,500,000. Ambazo ni sawa na asilimia 101.19 ya fedha iliyotakiwa kukopeshwa kwa vikundi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizungumza leo wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshmiwa Sospeter Nachunga amesema fedha hizo zimetolewa kwa vikundi 16 vyenye jumla ya wajasiriamali 155.
Amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa Halmashauri ya Mji Masasi ukilinganisha na hali ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Naishukuru sana serikali ya awamu ya tano imetuwezesha kusimamimia vizuri mapato jambo ambalo limeongeza uwezo wa wa Halmashauri kusaidia jamii. Tunaamini mwaka huu tutakuwa na mafanikio makubwa zaidi ya haya”. Alisema Mheshimiwa Nachunga.
Mheshimiwa Nachunga ambaye pia ni diwani wa kata ya Napupa amewataka vijana, akina mama, na walemavu kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili iwe rahisi kukopesheka.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mzee Mkongea Ali amepongeza hatua hiyo na kuwataka wajasiliamali walionufaika na mikopo hiyo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi.
Aidha, leo hii Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Mji Masasi umepitia miradi saba (7) ambapo katika miradi hiyo, mradi mmoja umefunguliwa, mradi mmoja umezinduliwa, miradi minne imeonwa na kukaguliwa, wakati mradi mmoja umewekewa jiwe la msingi.
miradi hiyo ina thamani ya shilingi 1,485,752,350.00 ambapo fedha kutoka Serikali kuu ni shilingi 445,652,350.00, Halmashauri shilingi 38,100,000.00, Wananchi shilingi 2,000,000.00, na sekta binafsi ni shilingi 1,000,000,000.00.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.