Mei 31,2019 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Zuena Ungele wakiambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya MJi Masasi Mhe.Sospeter Nachunga walikabidhi mkopo wa TZS.20,000,000/= kati ya TZS.58,000,000/= sawa na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Masasi kwa vikundi sita vya ujasiliamali katika mchanguo ufuatao. Kikundi cha Majesa Women Group kutoka Matawale TZS.3,000,000/=, Kikundi cha Upendo kutoka Mkomaindo TZS.3,000,000/=, Kikundi cha Tuleane kutoka Namkungwi TZS.2,000,000/=, Kikundi cha Neema kutoka Mtandi TZS3,000,000/=, Kikundi cha Amani kutoka Mkuti TZS.8,000,000/= na Kikundi cha Wachumi kutoka Mkuti TZS.1,000,0000/=
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi.Zuena Ungele alielezea kuwa mikopo hii ni utekelezaji wa sheria na ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Pia kaimu Mkurugezi aliendelea kufafanua kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ilitengwa bajeti ya TZS.202,355,270 kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake na walemavu sawa na asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya Halmashauri. Asilimia 10 ya pesa iliyokusanywa ni TZS 58,000,000/= na leo Mei 31, 2019 imetoka TZS. 20,000,000/ kati ya TZS.58,000,000/=
Vilevile Bi.Zuena Ungele alisisitiza vikundi vyote vilivyonufaika mikopo hiyo na kusema “hii ni mikopo na sio zawadi hivyo naendelea kusisitiza kufanya marejesho kwa wakati, pia naendelea kusisitiza wanavikundi kwamba tutakuwa tunawatembelea mara kwa mara” .
Wakati wa makabidhiano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Sospeter Nachunga alipokuwa akikabidhi hundi ya TZS.20,000,000/= kwa vikundi sita alisisitiza yafuatayo:
“Hili swala la Mikopo kwa vijana , wanawake na watu wenye ulemamavu ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi”
“Mikopo hii inatoka kila mwaka hivyo ni jukumu la wanavikundi kuomba mikopo kwa sababu siku hizi hakuna riba yoyote”
Mwisho Mhe. Mwenyekiti aliwapongeza wanavikundi kwa kitendo cha kujiunga na vikundi ili wapate mafanikio chanya ambayo yataweza kuwasaidia kumudu mahitaji yao.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.