Watumishi wa Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Reuben Sixbert Jichabu kwa kutatua changamoto mbalimbali za watumishi kwa wakati hali iliyopelekea kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kuwatumikia wananchi.
Wametoa pongezi hizo katika kikao maalumu kilichoongozwa na Mkurugenzi cha kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi wa Halmashauri ya Mji Masasi kilichofanyika Septemba 3, 2024 katika Ukumbi Mkubwa
wa Jengo la Utawala.
Wakizungumza katika kikao hicho wamesema utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa watumishi ikiwemo stahiki za watumishi umefanyika kwa kiwango kikubwa na hivyo kuongeza ari, ufanisi na Kasi ya utendaji.
“Mkurugenzi sote tumeshuudia hapa watumishi wanafuraha kwasababu changamoto zao unazitatua kwa wakati, uwazi na ufanisi, tunaomba uendelee na moyo huo huo, ufanisi wa watumishi umeongezeka, tunakuombea sana”., wamesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mji Masasi ameendelea kusisitiza watumishi kufanya kazi wa weledi, ufanisi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika kuwatumikia wananchi katika maeneo yao ya taaluma.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha maslahi ya watumishi yanatimizwa kwa wakati na ubora hivyo ataendelea kuhakikisha malengo ya Serikali yanatimia katika kuwatumikia wananchi kwa ubora na ufanisi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.