Kamati ya Fedha na Utawala ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba Oktoba 21, 2024 imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo imekagua jumla ya miradi Tano.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa mabweni mawili,madarasa manne,na matundu kumi ya vyoo shule ya Sekondari Temeke yenye thamani ya shilingi milioni mia tatu sitini na tisa,Ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo,shule ya msingi Sabasaba yenye thamani ya shilingi milioni Hamsini na nane na laki mbili,Ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo shule ya msingi Mkuti B yenye thamani ya shilingi milioni themanini na tatu na laki mbili,Ujenzi wa shule ya sekondari ufundi Marika yenye thamani ya bilioni moja na milioni mia sita na kituo cha Mazingira(ENZIKREIS) chenye thamani ya zaidi milioni mia mbili arobaini na mbili.
Akizungumza katika ukaguzi huo, Mhe. Namtumba amesema kwa kasi ya ujenzi wa miradi hiyo inaonyesha jinsi gani halmashauri ya Mji Masasi inafanya kazi kubwa sana katika kusimamia miradi kwa sababu miradi yote inaendana na muda na kwa kuzingatia ubora, kwa hiyo kasi hiyo iendelee kwenye miradi yote ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Masasi.
Aidha, Kamati hiyo imepongeza juhudi za Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada zake za kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi wa Masasi Mji sambamba na kutoa shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.