Kamati ya Fedha na Utawala ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba Oktoba 21, 2024 imetembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya ufundi Marika wenye thamani ya Tsh bilioni 1.6 unaojengwa katika Kata ya Marika Halmashauri ya Mji Masasi.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Namtumba amesema ujenzi wa shule hiyo ya kipekee unaenda kuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Masasi kwa sababu itaenda kunufaisha vijana kwa kuwapa ujuzi ambao utasaidia kuongeza ajira.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema atahakikisha miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kwa ubora na kuikamilisha kwa wakati.
Kamati hiyo imepongeza juhudi za Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada zake za kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi wa Masasi Mji sambamba na kutoa shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.