Mkurugenzi wa Mji Masasi bi Erica Yegella kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Mtandi halmashauri ya Mji Masasi wamepanda miti ya Matunda aina ya parachichi na vivuli katika Eneo la shule ya Msingi Mtandi.
Zoezi hilo limefanyika agosti 16,2023 likiwa na lengo la kuboresha Mazingira kwa maeneo ya Halmashauri ya Mji Masasi.
Sambamba na hayo Bi.Erica Yegella amewapongeza viongozi na wananchi wa kata ya Mtandi kwa kuanzisha zoezi la upandaji miti katika Shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo kata ya Mtandi.
“Hongereni wananchi na Viongozi ambao mnaongozwa na Mh.Diwani ambaye yeye ndiye anaetekeleza ilani ya chama chama cha Mapinduzi leo tumepanda Mtandi shule ya Msingi na nipongeze kwa kuanzisha zoezi hili mimi kama Mkurugenzi naahidi kutoa ushirikiano kwa watendaji wa vijiji,kata na mitaa na nitakuwa natoa tuzo kwa watendaji watakaofanya vizuri na kazi bora”
Kwa upande wake Meneja tawi Masasi Davis Minja ambaye pia ni mgeni Rasmi wa zoezi hilo ameeleza kuwa Benki ya Nmb imekuwa ikiendesha kampeni ya utunzaji wa Mazingira katika maeneo mbalimbali Tanzania.
“Bank ya Nmb tumekuwa tukiendesha kampeni ya upandaji miti katika maeneo tofauti na halmashauri ya Mji masasi tumepanda miti zaidi ya 1000 na nafurahi kuona zoezi hili na jitihada hizo zinazidi kuwa endelevu kwa maana sasa tunazidi kuboresha Mazingira na ahadi yetu ni kwamba tutazidi kushirikiana na Mkurugenzi wa Mji Masasi katika Shughuli mbzlimbali za Maendeleo” Davis Minja Meneja Nmb tawi Masasi.
AKitoa taarifa ya upandaji Miti Mtendaji kata ya Mtandi Kahinda Kahinda ameeleza kuwa wamepanda miti zaidi ya 60 katika eneo hilo na zoezi hilo litakuwa endelevu kwa kata ya Mtandi.
Aidha Kahinda amesema kuwa kata hiyo ina mpango wa kuanzisha vitalu vya uzalishaji wa miche ya aina mbalimbali.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.