Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi likiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Sospeter Nachunga limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Reuben Sixbert Jichabu kwa kununua kifaa kipya cha upimaji wa ardhi (RTK) na kupeleka fedha za mapato ya ndani kwenye miradi yote iliyotengewa fedha kwa mwaka 2025/2026.

Wakizungumza katika Mkutano wa Baraza uliofanyika Desemba 02, 2025 wametoa pongezi hizo kwa Mkurugenzi wa Mji na Menejimenti baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Halmashauri katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilikuwa limevunjwa.
“Ukisoma na kupitia taarifa hii unaona mambo makubwa yamefanyika kwaajili ya wananchi wetu kwa mfano kuna ununuzi wa kifaa cha RTK tulitenga kwenye bajeti hii milioni 50 lakini Mkurugenzi Kanunua kwa milioni 45 tu, nipongeze sana maana wananchi sasa wanakwenda kupimiwa maeneo yao ili wapate umiliki wa hati kwa haraka na urahisi, lakini pia miradi ya maendeleo tuliyoitengea fedha kwakweli yote unaona kuna fedha zimeshapelekwa na mingine imeshaanza kutekelezwa” wamesema.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.