- Madiwani waapishwa kuanza kazi
- Mhe. Sospeter Pesivo Nachunga achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri
-Mhe. Omari Saidi Omari amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
- Kamati za kudumu zaundwa
Mkutano wa kwanza wa Halmashauri ya Mji Masasi umefanyika Desemba O2, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo Madiwani wameapishwa tayari kuanza majukumu yao kwa kipindi cha Miaka Mitano.
Katika Mkutano huo umefanyika Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Bi. Fatima Kubenea alimtangaza Mhe. Sospeter Pesivo Nachunga, Diwani kata ya Napupa kuwa mshindi wa nafasi mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi baada ya kupata kura zote 19 za Ndio.
Aidha Mhe. Omari Saidi Omari amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kamati za kudumu za Halmashauri zimeundwa huku Mheshimiwa Mwenyekiti akitaja vipaumbele vyake ikiwemo ukusanyaji wa Mapato ya ndani, uwajibikaji na mahusiano bora kati ya Watumishi na Waheshimiwa Madiwani.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Rachel Kassanda amewapongeza waheshimiwa madiwani kwa kuchaguliwa huku akiwahimiza kwenda kuhamasisha usafi wa mazingira kwenye kata zao.
Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema wanakwenda kutoa ushirikiano bora kwa Baraza hilo na kutekeleza maagizo na ushauri wowote wenye tija kwa wananchi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.