Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu ametangaza rasmi maboresho mbalimbali ya huduma kupitia Mapato ya ndani katika hospitali ya Mkomaindo ambazo sasa zinatolewa wakati wote baada ya kupata madaktari bingwa wa kudumu Hospitali ya Mkomaindo.
Ametangaza huduma hizo wakati akizungumza na wafanyabiashara soko la Mkuti kama ifuatavyo;
Huduma za kibingwa za MIFUPA katika Hospitali ya Mkomaindo zimeanza rasmi kutolewa na Daktari Bingwa akiwa na Vifaa tiba vya kisasa vilivyonunuliwa kupitia mapato ya ndani.
Kuanzisha Huduma za Mazoezi Tiba (Physiotherapy) katika Hospitali ya Mkomaindo ambapo jengo limekarabatiwa na vifaa tiba vya kisasa vimenunuliwa kupitia Mapato ya ndani ya Hospitali.
Kuboresha kitengo cha Huduma za Macho katika Hospitali ya Mkomaindo ambapo jengo limekarabatiwa na vifaa tiba vya kisasa vimenunuliwa kupitia Mapato ya ndani ya Hospitali.
Ujenzi wa Wodi ya Kisasa kwaajili ya wateja maalumu VVIP katika Hospitali ya Mkomaindo kupitia Mapato ya ndani ya Hospitali ambapo ujenzi umeanza kutekelezwa.
Aidha amesisitiza kuwa maboresho yanakwenda kufanyika kwenye UTOAJI WA HUDUMA kwa wagonjwa ambapo Watalaam bobevu wa Huduma kwa wateja wanakwenda kutoa mafunzo elekezi kwa wahudumu wote Hospitali ya Mkomaindo ili maboresho na huduma zilizofanyika ziende sambamba na huduma bora.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha wananchi wa Halmashauri ya Mji Masasi wanapata huduma za kibingwa kwa urahisi, ubora, ufanisi na haraka.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.