Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi Mariamu Chaurembo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta amewaomba wasimamizi wa ukusanyaji wa Mapato Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara kuzingatia Matumizi ya Mashine ya POS kwa maeneo yote ya ukusanyaji wa mapato na kuwasimamia wakusanyaji wa mapato hayo kwa kufuata sheria ili Mapato yaweze kuongezeka katika Halmashauri hiyo.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupiitia na kujadili Rasimu ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 uliofanyika Januari 21,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Masasi.
Aidha Bi Chaurembo amewapongeza Madiwani na wataalam wote kwa kufanya kwa asilimia 100 ,hivyo amewashauri kuwa timu moja ili kurahisisha utendaji kazi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendelei ya Halmashauari ya Mji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bi Mariam Kasembe ametoa pongezi kwa Menijimenti yote kwa kuzingatia vipaumbele Muhimu na vinavyogusa maslahi ya wanajamii wa Masasi kwa kupitia bajeti iliyotengwa ya mwaka 2023/2024 kwani ni moja ya mafanikio katika Maendeleo.
Bajeti ya Halmashauri ya Mji Masasi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imekisia kukusanya na kupokea jumla ya Shilingi 24,015,608,000.00 kati ya fedha hizo Mapato ya Ndani ni Shilingi 2,855,980,500.00 Ruzuku na Matumizi ya kawaida na Mishahara ni Shilingi 15,737,987,000 na Miradi ya Maendeleo ni Shilingi 8,277,621,400.00 .
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.