Kamati ya fedha,Utawala na Mipango julai 24,2023 wamefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo mbalimbali ambayo inatekelezwa na Halmashauri ya Mji ya Masasi.
Kamati imekagua miradi ya ujenzi wa Miundo ya Shule kupitia Mradi wa Boost ,Ujenzi wa Miundo mbinu ya Hospitali ya Mkomaindo,Ukarabati wa Kituo cha Walimu Mkomaindo(TRC),Ujenzi wa Uzio wa Shule ya Watoto wenye Mahitaji Maalum Masasi kata ya Mtandi,Ujenzi wa vyumba 9 vya Madarasa Shule ya Msingi Migongo na ofisi na Ujenzi wa Mabweni mawili ,Vyumba vya Madarasa tano na Matundu Saba ya vyoo Shule ya Wasichana Masasi (Masasi Girls).
Kupitia Ziara hiyo Mjumbe wa kamati ya fedha ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Ndg. Geoffley Mwambe ametoa pongezi kwa Diwani na wananchi wa kata ya Mkomaindo kwa kujitolea nguvu kazi na kuhakikisha ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi yenye Mkondo Mmoja inakamilika.
‘’Hongera saana Mhe. Diwani pamoja na wananchi wako kwa kujitolea kufanya kazi katika eneo la Shule hii hadi kuhakikisha mnakamilisha kwa wakati hakika tunakila wajibu wa kuwapongeza kwa juhudi mlizozionyesha’’Mwambe
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.