Zaidi ya Shilingi Milioni Miatisa (900) kutekeleza Miradi Mia Moja (100) ya Ajira Kwa Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF.Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 imeanza Utekelezaji wa Ajira za Muda Kwa Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF ,na Miradi hiyo inatekelezwa katika Vijiji 88 ambavyo vinaumda Halmashauri ambapo Miradi Mia Moja (100) Tayari imeanza kutekelezwa.
Miradi ambayo inatekelezwa ni Miradi Nane ya Utunzaji wa Mazingira na Upandaji Miti ambapo Miti Elfu Sita Mia Tisa Thelathini na Mbili (6932) inatarajiwa kupandwa ,Miradi Ishirini (20) ya Uvunaji wa Maji ya Mvua na Ujenzi wa Matanki ya Chini katika Taasisi ikiwemo Mashuleni na Zahanati Vilevile Miradi Sabini na mbili (72) ya Ufunguzi na Utengenezaji wa Barabara za Jamii yenye Urefu wa kilometa 434.571.
Katika Miradi hii Jumla ya kaya 4464 zinatarajiwa kunufaika Moja Kwa Moja Kwa kushiriki kazi na kulipwa Ujira.Miradi hii imeanza kutekelezwa November 2,2022 katika Vijiji na Mitaa 40 ambayo ni Vijiji vya Zamani na Mitaa arobaini na Nane (48) Mipya bado haijaamza kutekelezwa na Thamani ya Miradi tote inayotekelezwa ni zaidi ya Shilingi Milioni Miatisa (900).
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.