Diwani kata ya Napupa halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Sospeter Nachunga amewaomba wazazi na walezi wa shule ya msingi Kambarage na kata ya Napupa kiujumla kuchangia upatikanaji wa chakula shuleni ili kukuza maendeleo ya elimu.
Ameeleza hayo Oktoba 18,2023 katika kikao cha wazazi kilichofanyika Shule ya Msingi Kambarage na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama cha mapinduzi, Walimu, Afisa elimu ya awali na msingi, wazazi, wanafunzi na wadau mbalimbali.
Mhe. Nachunga ameeleza kuwa chakula kikitolewa Mashuleni kitaongeza ufaulu ,watoto watapenda shule na Maendeleo ya elimu yataongezeka zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Afisa Tarafa halmashauri ya Mji masasi, Ndg. Fikiri Lukanga amewaomba wazazi kuona umuhimu wa kuchangia chakula Shuleni kwa ajili ya utekelezaji wa lishe bora ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi .
Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Mji Masasi Bi. Hamida Msemo amesema kikao hicho kina lengo mahususi la kuhamasisha wazazi kuchangia upatikanaji wa chakula Shuleni.
Naye, Mzazi na Mkazi wa Kata ya Napupa, Ndugu. Juma Mtinga amesema kama wazazi wana jukumu la kuhakikisha kila mzazi anachangia chakula ili wanafunzi wasome kwa bidii wakiwa shuleni.
“kila mzazi anatakiwa kuchangia chakula Shuleni na sio serikali "Ndg. Mtinga
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.