• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe za Watumishi |
Masasi Town Council
Masasi Town Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisa Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Mji Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Fedha
    • Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Biashara
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Utawala na Utumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango miji na mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

WATOTO ZAIDI YA 200 WAPATA ELIMU YA LISHE, WANAUME WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI

Posted on: August 16th, 2023

Zaidi ya watoto 200 wamepata elimu ya Lishe bora kutoka vijiji vya Mayula na Mbonde kata ya Mwenge Mtapika Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Agosti 16, 2023, Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Masasi, Bi. Happiness Mlamka amesema lengo mahususi la elimu hiyo ni kuwakumbusha wazazi, walezi na jamii juu ya umuhimu wa afya na lishe kwa mtoto.

“kipekee kabisa tumekuja kwenye adhimisho la siku ya afya na lishe ya Kijiji. Siku hii imelenga kuwakumbusha wazazi, walezi na jamii kwa jumla juu ya umuhimu wa afya na lishe kwa mtoto lakini pia kwa jamii nzima, mambo yaliyofanyika leo tumetoa elimu juu ya unyonyeshaji wa Watoto kwa miezi sita hadi miaka miwili, lakini pia tumetoa elimu ya makundi Matano ya chakula, namna sahihi ya kuandaa mlo kamili kwa vile vyakula vinavyopatikana katika jamii kwa vitendo” Bi. Mlamka

Aidha amesisitiza umuhimu wa wanaume kuhudhuria matukio ya elimu ya afya na lishe  kwa kuwa ni jukumu la wazazi wote kuhakikisha lishe bora inapatikana.  

“leo tumepata baadhi ya wanaume, tunaendelea kutoa wito wanaume wote tuendele kujitokeza kwa kuwa zoezi hili ni la wote” Afisa lishe.

Kwa upande wake, Afisa mtendaji wa Kijiji cha Mayula Bw. Alex Mwambwalwa amesema idadi ya wazazi waliofika katika elimu hiyo imefanikiwa kutoka na uhamasishaji uliofanyika na mwamko wa wazazi juu ya umuhimu wa lishe kwa Watoto.

“wananchi tulionao hapa wanatoka katika Kijiji cha Mayula na Kijiji cha Mbonde na Idadi ya Watoto waliohudhuria ni takribani Watoto 200” Bw. Alex

Mmoja kati ya baba aliyefika akiwa na mtoto wake kupata elimu hiyo, Bw. Samweli Abdalah mkazi wa Kijiji cha Mayula, amewahimiza wazazi wa kiume kujitokeza kwa wingi katika matukio ya elimu za afya na lishe zinazotelewa na watalaamu ili kuwezesha malezi bora ya Watoto.

“ Mimi natokea kata ya Mwenge mtapika, kijiji cha Mayula, nimekuja kujifunza juu ya kumlea mtoto kuhusu uji wa lishe, nawakaribisha wazazi wenzangu jukumu la kumlea mtoto sio la wanawake pekee yake, tujitahidi sana kuhudhuria sana kwenye hii mikusanyiko, tunajifunza mambo mengi sana” Bw. Samweli.

Katika kuhakikisha  lishe bora inapatikana utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa chakula shuleni unatekelezeka kwa vitendo katika kata hiyo ikiwemo kupata mafanikio katika shule ya msingi  Mbonde kwa kulima, kuvuna na kukusanya mazao kama mbaazi, mahindi na alizeti.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI July 28, 2020
  • TANGAZO LA KAZI April 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • Kuona Vyote

Habari Mpya

  • “VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MTWARA TUWEKE KIPAUMBELE CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA OKOVU NA HUDUMA MSINGI KWA WAGONJWA MAHUTUTI” RAS MTWARA.

    May 15, 2025
  • “WANANCHI TUJITOKEZE MKOMAINDO HOSPITALI KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA SARATANI BURE, SERIKALI IMELIPIA GHARAMA (SAMIA SULUHU OUTREACH SERVICES)” DC KASSANDA

    April 23, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA MASASI MJI, ZAIDI YA MILIONI 545 ZATOLEWA MWAKA HUU WA FEDHA 204/2025 KWA VIKUNDI 105 MIKOPO YA ASILIMIA 10.

    April 07, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA MASASI MJI WATOA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA MPOX

    April 06, 2025
  • Kuona Vyote

Video

SHERIA ZA MITANDAO
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Sheria ndogo ya Ada na Ushuru kwa Mji wa Masasi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Mtwara
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais UTUMISHI
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • SALARY SLIPS PORTAL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    MASASI TOWN COUNCIL

    Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI

    Simu Ya Mezani: +255 23 2510685

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: info@masasitc.go.tz

Mawasiliano

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.