Jumla ya watoto elfu Ishirini na Nne Mia Saba na Sitini na tisa (24,769) Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara wanatarajia kupata chanjo ya polio katika kampeni ya kitaifa ya awamu ya Nne ambayo inatarajia kuanza December 1,2022 na kumalizika December 4,2022.
Mratibu wa chanjo halmashauri ya Mji Masasi Josephu Stanley Njuyuwi amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa kawa kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (5) ambao waliowahi kupata chanjo zilizopita na wasiopata kabisa.
Ameeleza hayo katika kikao cha kamati ya chanjo ya msingi wilaya ya Masasi kilichofanyika November 30,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Masasi.
Josephu Stanley ametolea ufafanuzi kwa kampeni ya chanjo iliyopita ya awamu ya tatu ambayo ilifanyika September I ,2022 hadi September 4 1,2022 amesema kuwa Halmashauri ya Mji Masasi ililenga kutoa chanjo ya polio 17,903 ,idadi ya chanjo zilizotumika ni 24,769 na idadi ya watoto waliochanja ni 24,769 sawa na asilimia 138.
Pia amesema chanjo ya Polio ya awamu ya Nne kamati imejipanga vizuri imeongeza timu ambayo itapita nyumba hadi nyumba na maeneo yote ambayo yametengwa kwa ajili ya kutolea huduma hiyo na kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anapata chanjo.
Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Masasi Claudia kitta ametoa wito kwa wazazi na walezi wote khakikisha wanawapeleka watoto wao kwenda kupata chanjo ya polio katika maeneo yaliyotengwa yakutolea huduma ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali ambayo ni rahisi kwa mtoto kuambukizwa
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.