Wazee wanufaika wa TASAF Halmashauri ya Masasi Mji wampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bi Erica Yegella kwa utendaji wake kazi baada ya kuita kwenye kikao chake na Wazee leo Julai 14'2023.
Kikao hicho kimehudhuriwa na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Mtwara Cde Julius Kaondo, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mheshimiwa Geofrey Mwambe pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Masasi Bi Fatma Kubenea.
Hayo yamesemwa na Wazee wanufaika wa TASAF ambao wamekiri kuwa ni mara yao ya kwanza kuwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Masasi Mji aliweza kuwaita na kufanya nao mazungumzo.
Katika kikao hicho Mkurugenzi Bi Erica Yegella ameleza lengo la kikao hicho kupata uelewa wa kuhusu TASAF na namna Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inavyowajibika na kutekeleza majukumu yake ikiwemo kwa wanufaika wa TASAF.
Aidha kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha TASAF Halmashauri ya Masasi Mji ndugu Amiry Nyiruka mpaka sasa zaidi ya walengwa 5431 wa TASAF wamenufaika na afua mbalimbali za miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Julius Kaondo amewataka Wazee hao kutambua jitihada za Serikali inaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan inavyowajibika kutatua na kusaidia jamii ya wana TASAF.
Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Masasi Bi Fatma Kubenea amewataka waxes hao kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan ikiwa pamoja na Kumuombea ili aweze kuendelea kuwatumikia Wazee hao.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.