Wananchi wa Kijiji cha Nangose kilichopo Kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi wametoa shukrani zao za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Gasper Byakanwa kwa msaada wa vifaa vya ujenzi ambavyo wamekabishiwa leo hii na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimiwa Selemani Mzee Kijijini hapo ikiwa ni kuwaunga mkono kwenye utekelezaji wao wa Kampeni ya Shule ni Choo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tatu laki nne na ishirini na sita elfu (3,426,000) shuleni hapo leo Jumamosi ya tarehe 07/12/2019.
Akongea kwenye makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Masasi amewapongeza Wananchi hao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuchanga kiasi cha shilingi milioni moja, laki mbili, na themanini elfu (1,280,000) iliyowezesha kujenga vyoo hivyo ambapo matundu kumi ya vyoo yamefikia hatua ya renta wakati matundu tisa yamefikia kozi nne hadi leo, Ujenzi huo umefanyika kwa matofali ya saruji.
Mheshimiwa Selemani Mzee amewataka wananchi hao kutilia maanani umuhimu wa Elimu kwa watoto kwa kuwa ndicho chanzo pekee cha uwekezaji kwa maendeleo ya Taifa la kesho, huku akiwasisitiza Walimu kufanya kazi kwa bidii ili Wanafunzi wao wapate Elimu lengwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na taifa la kesho.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.