Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Prophina Machi 21, 2025 wametembelea kituo cha kutolea elimu ya mazingira Halmashauri ya Mji Masasi kwa lengo la kujifunza uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo Meneja wa Kituo cha Kutolea elimu ya Mazingira, Bi. Catherine Tendeje amesema watoto ni kizazi bora cha kesho hivyo ni muhimu kupata elimu ya uhifadhi wa mazingira wakiwa watoto.
“watoto hawa wamejifunza mambo mbalimbali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kupitia picha mbalimbali zilizopo katika kituo chetu, wamejifunza pia namna ya utunzaji wa miti ya matunda, kivuli na urembo.
Aidha Bi. Catherine ametoa rai kwa shule binafsi na za Serikali kutembelea kituo hicho kwa ajili ya kujifunza elimu ya mazingira itakayosaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Prophina Mwl. Reeves Oliver amesema kuwa wao kama shule wamejifunza mambo mengi sana ikiwemo umuhimu wa kutunza mazingira pia madhara yanayoweza kutokea endapo mazingira yataharibiwa na namna gani mazingira hayo yanaweza kutunzwa.
Kituo cha Elimu ya Mazingira ni mradi wa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Mji Masasi na Wilaya ya Enzkreis ya Nchini Ujerumani unaotekelezwa kwa malengo ya kutoa Elimu ya mazingira kwa vitendo kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari, Vyuo na Jamii kwa ujumla.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.