Wakazi wa Kijiji Cha Nangose kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara wametoa Shukrani Kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kuwapatia Mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf kwani umeweza Kuwainua Kiuchumi katika Maisha yao.
Shukran hizo zimetolewa November 23,2022 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji Cha Nangose kata ya Temeke na Mh Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Jenesta Mhagama katika ziara yake ya kuona na kukagua utekelezaji wa Miradi ya Ajira za Muda inayotekelezwa na Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF.
Gabliel Joshua Mkazi wa Kijiji Cha Nangose Kwa niaba ya wakazi hao ameeleza kuwa TASAF imewainua kiuchumia wameweza kuwasomesha watoto wao ,kupata chakula Kwa uhakika ,kupata Matibabu ya uhakika na kuanzisha Shughuli za Kiuchumi ambazo zitawasaidia kuendesha Maisha yao ya kila Siku.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.