Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi likiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Hashim Namtumba limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayowezesha ukuaji na ustawi wa wananchi wa Mji wa Masasi.
Aidha limemshukuru Mhe, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe kwa kupambana na kuhakikisha miradi ya maendeleo inawafikia wananchi katika kata zote 14 za Halmashauri ya Mji Masasi.
Hayo yamebainishwa Novemba 8, 2023 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya Kwanza, 2023/2024 wa kupokea taarifa za kata uliofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala Halmashauri ya Mji Masasi.
Wajumbe wa kikao hicho waheshimiwa madiwani wa kata wameelezwa kuwa miradi mbalimbali katika kipindi cha Robo ya kwanza imeendelea kutekelezwa kwa kasi ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari kata ya Jida, Ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo shule ya msingi Mkomaindo, Ujenzi wa bwalo, madarasa na vyoo shule ya sekondari Mwengemtapika, ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Temeke, ukamilishaji wa zahanati ya Napupa, ukamilishaji wa zahanati ya Matawale na Ujenzi wa Daraja Kata ya Marika.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hashim Namtumba amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakuza Mji na kuimarisha maendeleo ya wananchi kiuchumi na kijamii.
" Taarifa ya kata ya Marika imewasilishwa na Diwani wa kata Mhe Asha Millanzi, Kiupekee kuhusu daraja linalounganisha kati ya Nanyumbu na Masasi naomba tumpongeze sana Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe Geoffrey Mwambe kwa namna ambavyo amepambana kuhakikisha daraja lile linakuwepo, kwanza ni daraja kubwa sana, linatufungulia mlango wa mapato na kwa umuhimu wake lile daraja kwa halmashauri yetu ni mlango wa uchumi kwasababu mazao yote"
Naye, Diwani Kata ya Mwengemtapika Mhe. Mussa Millanzi ameshukuru kwa kupata fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata yake.
"Mhe Mwenyekiti napenda nishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya mama yetu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kiasi cha Tsh milioni 320 Mwengemtapika sekondari kwa ajili ya ujenzi wa bwalo, madarasa na vyoo ikiwa ni kuhakikisha shule ile inaenda kutimiza lengo la Halmashauri ya Mji Masasi kuwa na shule ya kidato cha tano na sita".
Aidha, Diwani kata ya Mkomaindo Mhe. Ally Salvatory amewashukuru wananchi kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
"Shule ya Msingi Mkomaindo kuna madarasa mawili yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi yameshafikia pamoja na hilo nishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kiasi cha Tsh milioni 208 za ujenzi wa maradasa 9 na matundu ya vyoo 16 na ujenzi upo kwenye hatua za ujenzi wa ukuta" Diwani kata ya Mkomaindo Mhe.
Mkurugenzi wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema Malengo ya Halmashauri ni kukusanya mapato kwa wingi ili utekelezaji wa miradi ya maendeleo uweze kutekelezeka kwa ubora na wakati ili wananchi huduma.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.