Mshauri wa Kifua Kikuu Mkoa wa Mtwara Dkt. Ben Saimon kwa niaba ya Mganga mkuu wa Mkoa na USAID Afya yangu amekabidhi kitendea kazi aina ya laptop kwa Mganga mkuu Halmashauri ya Mji Masasi Dkt. Salum Gembe ili kusaidia utendaji kazi wa uratibu na utoaji wa taarifa mbalimbali kuhusu huduma za Kifua kikuu na Ukimwi.
Akikabidhi kitendea kazi hicho Oktoba 5, 2023 Dkt Ben amesema Usaid Afya yangu kanda ya kusini inazisaidia halmashauri katika mkoa kwa kutoa vitendea kazi ili utoaji, uratibu na uwasilishaji wa taarifa mbalimbali za Kifua kikuu na Ukimwi zifanikiwe kwa ufanisi uliokusudiwa.
“ Kitendea kazi hiki kitasaidia katika uratibu wa kupambana na kifua kikuu, Kwa kuhakikisha ripoti na taarifa za wagonjwa zinaingia na kujazwa kwa wakati kwenye mfumo” Dkt Ben.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Mji Masasi Dkt. Salum Gembe amewashukuru USAID afya yangu kwa kutoa kitendea kazi hicho na kuahidi kuwa kitasaidia vyema katika utoaji wa taarifa za Kifua kikuu kwa wakati na ufanisi uliokusudiwa.
"Tunashukuru sana kwa kutukabidhi kompyuta, Sisi kama Masasi Mji tunashukuru sana kwa msaada wenu na sisi tunawaahidi kitendea kazi hiki kitafanya kazi na kutoa data ambazo ni halisia, ambazo zitatuinua katika kuwasilisha data zetu, kama Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe tutaendelea kupambana na Kifua kikuu na Ukimwi"
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.