Mkurugenzi wa Mji Masasi Bi.Erica Yegella Julai 27,2023 ametembelea Kituo cha Afya Mtandi kilichopo Halmashauri ya Mji - Masasi kwa lengo la kuona namna ya utoaji huduma na kuzungumza na wananchi ambao wanapata huduma katika Kituo hicho.
Kwa upande wao wananchi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha ambazo zimewezesha kujenga Miundo mbinu ya Afya kwani imesaidia kupunguza kutembea umbaali Mrefu kwenda hospital ya Mkomaindo kufuata huduma ya Afya.
"Tunashukuru kwakweli kwa kupata kituo hiki maana tulikuwa tunatembea umbali Mrefu kwenda Mkomaindo kufata huduma hii lakini sasa Rais Samia ametuokoa kwakweli tunapata tiba karibu na yenye ubora "
Mkurugenzi wa Mji Masasi amewaomba wananchi hao kuwa na amani na kutoa taarifa pale changamoto zinapojitokeza.
"Kuweni na amani mnapokuja kupata huduma katika kituo hiki na yeyote atakaepata changamoto ya upatikanaji wa huduma atoe taarifa na mnalojukumu la kutunza Miundo mbinu ya kituo hiki"Erica Yegella
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.