Mkuu wa wilaya ya Masasi Lauter Kanoni ametoa agizo kwa Taasisi binafsi kushirikiana na Serikali kutokomeza vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea katika jamii zetu na kutoa taarifa kwa wakati pale matukio ya kikatili yanapotokea ili yaweze kufanyiwa kazi .
‘’Toeni taarifa kwa wakati sahihi pale tu matukio ya ukatili yanapotokea ili yaweze kushughulikiwa kwa wakati na niwaombe wazazi kuonyesha ushurikiano pale changamoto za uikatili zinapotokea ‘’Kanoni.
Ameeleza hayo katika hafla ya Maadhimisho ya sherehe za siku ya wanawake duniani ambyo kwa halmashaurio ya Mji Masasi yamefanyika March 4,2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondario ya kutwa Maili sita kata ya Chanikanguo ambapo taasisi mbalimbali walihudhuria hafla hiyo.
Aidha Kanoni kupitia Maadhimisho hayo aliwaomba wanawake ,kuunda vikundi na kuvisajili ili waweze kupatiwa Mikopo wa asilimia kumi wa mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo yanatolewa kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu na kuhakikisha mikopo hiyo wanairejesha kwa wakati na wengine waweze kukopeshwa.
‘’Serikali imetenga fedha yanayotokana na mapato ya Ndani kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi kwa kufuata kanuni na taratibu za utoaji Mikopo hiyo hivyo basi undeni Makundi ,fuata taratibu zote ili muweze kuwa na vigezo vya kukopeshwa fedha hizi kwani Serikali inalengo la kuwainua wananchi wake na hakikisha mnakuwa na biashara ambayo itakuingizia kipato kuepusha changamoto wakati wa marejesho kopeni na rejesheni kwa wakati na wengine waweze kukopeshwa’’Kanoni.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.