WALIMU wanaofundisha masomo ya sayansi katika Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kuwalea vizuri na kuwavumilia watoto wanaowafundisha masomo hayo ili wayapende na kuja kuwa na wanasayansi bora.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Mji wa Masasi , Erica Yegella wakati akizungumza na walimu 126 wa masomo ya sayansi ambao wanapatiwa mafunzo endelevu kazini ili waweze kufundisha watoto kwa ufanisi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Masasi,Erica Yegella akizungumza na walimu wa masomo ya sayansi wa halmashauri hiyo katika shule mpya ya Mkomaindo ambao wanapatiwa mafunzo ya elimu endelevu kazini
‘’Niwaombee heri katika siku hizi mbili za mafunzo yenu ,mimi huwa naheshimu sana walimu wa shule za msingi kwasababu yeye ndiye msingi kuanzia awali ,msingi mpaka darasa la saba nyie dira ya maisha maana nyie ndo mnatoa viongozi ,wakurugenzi ,mkuu wa wa wilaya , mwalimu bora,”amesema na kuongeza kuwa
“Nina hakika mtakuwa walimu bora na si bora mwalimu ufanisi wenu na ubunifu wenu na utendaji kazi katika kufundisha watoto wetu bila kuogopa masomo nautegemea sana ‘’amesema Mkurugenzi huyo
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.