Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi, Mhe. Hashim Namtumba amewataka wakuu wa idara, vitengo na wataalamu kutekeleza wajibu wao kwa weledi na ufanisi ili kuchochea maendeleo ya halmashauri.
Amesema wataalamu wanatakiwa kuwa na uhalisia katika ukadiliaji wa fedha katika miradi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Mhe. Namtumba amesema hayo agosti 3, 2023 katika mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya nne 2022/2023 uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la Utawala.
“Mkurugenzi hoja hapa tuliyonayo ni kwamba hatujawahi kuona fedha zinabaki kwenye mradi, kila mradi fedha hazitoshi hasa miradi inayotekelezwa na fedha kutoka serikali kuu” Mhe. Namtumba
Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kwenda kusimamia eneo la ukamilishaji wa miradi ili kuondoa changamoto iliyopo ya kutokamilisha miradi kwa fedha zilizotengwa kwenye mradi husika.
“Mkurugenzi hili ni baraza lake la kwanza ni vizuri sasa tukianza pamoja ili turuke pamoja, ukasimiamie eneo la ukamilishaji wa miradi ili tusiwe na miradi isiyokamilika” amesema.
Katika hatua nyingine amesema Baraza la Madiwani linamkaribisha Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Bi. Erica Yegella kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki katika mkutano wa Baraza la Madiwani.
Amesema waheshimiwa madiwani kwa pamoja wanamkaribisha mkurugenzi katika halmashauri hiyo na kwamba wapo tayari kwa dhati kushirikiana naye ili kuendeleza ustawi wa maendeleo ya halmashauri.
Mkutano wa baraza hilo ulihudhuriwa na waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara na vitengo, wakuu wa taasisi mbalimbali, viongozi kutoka vyama mbalimbali, viongozi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa na wadau mbalimbali.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.