Takwimu za utoaji wa huduma za afya zimetakiwa kutumika kama dira na mwongozo kwa watoa huduma za afya katika kufanya tathmini ya utoaji wa huduma bora za afya mara baada ya kiwango cha utumaji wa taarifa za afya (MTUHA) kuongezeka kutoka asilimia 96.56 hadi 98.98 katika kipindi cha Januari- Machi 2024 Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Akizungumza April 29, 2024 katika Kikao kazi cha kujadili takwimu za huduma za afya kwa kipindi cha Oktoba- Desemba 2023 na Januari - Machi 2024, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Andrea Kalinga amesema Takwimu zitumike kufanya tathimini ya hali ya utoaji wa huduma kwa kujipima utendaji kazi na huduma zinazotolewa na watoa huduma kwa kuzingatia taratibu, miiko na maadili ya kazi.
" Tathmini hii tunayoifanya naomba iwe ni dira, mwongozo, taa kwetu kuona pamoja na kwamba tunafanya tathmini kama kituo lakini tufanye tathmini ya mtu mmoja mmoja jinsi anavyotoa huduma kwenye sehemu yake ya eneo analolitolea huduma" Kaimu Mkurugenzi.
Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Salum Gembe amesema lengo kuu ni kujadili takwimu za afya MTUHA huku malengo mahususi yakiwa ni kutambua ubora wa takwimu za afya, kutambua kiwango cha ufanisi wa utoaji wa huduma za afya, kubainisha changamoto zilizopo katika takwimu za afya na kuweka mikakati ya pamoja ili kuboresha huduma.
“Hali ya utumaji wa taarifa za MTUHA kutoka vituoni. katika kipindi cha Oktoba - Desemba kiwango cha utumaji wa taarifa ni asilimia 96.56, taarifa zilizotumwa kwa wakati zilikuwa asilimia 95.96 na Januari- Machi kiwango cha utumaji wa taarifa kilikuwa asilimia 98.98, zilizotumwa kwa wakati 95.52, kiwango cha utumaji wa taarifa kimeongeza kutoka asilimia 96.56 hadi 98.98 Januari- Machi 2024”, amesema Dkt Gembe.
Kikao kazi hicho kimehusisha wajumbe wa timu ya usimamizi CHMT, waganga wafawidhi kutoka vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali na vituo Binafsi (vyote 23) na wataalamu mbalimbali wa afya.
Matukio katika picha.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.