Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara ilitangaza rasmi kuanza kutumika kwa standi yake mpya ya Maegesho ya vyombo vya moto (Magari) March 17, 2025 iliyopo Kata ya Mwengemtapika barabara ya kuelekea Tunduru ambapo mwamko wa kupeleka na kulaza vyombo vya moto umekuwa mkubwa na umeleta fursa mpya kwa wananchi wa Masasi wakiwemo Mama Ntilie, Wafanyabiashara na Maafisa usafirishaji wa Pikipiki (bodaboda).
Katika picha ni March 22,2025 wananchi wakiwa katika maandalizi ya fursa mbalimbali katika eneo hilo na magari yanayoendelea kuegeshwa katika standi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Andrea Kalinga alisema ujenzi wa standi hiyo umeleta suluhu ya kuondoa msongomano wa vyombo vya moto kupaki kiholela katika maeneo ya mjini.
Nayo, Kamati ya Fedha na Utawala ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Hashim Namtumba ilitembelea na kukagua standi mpya ya maegesho ya vyombo vya moto (magari) sambamba na vituo vya mafuta mbalimbali ambapo wamewasisitiza wamiliki wa vituo vya mafuta kuhakikisha magari hayalazwi katika vituo vyao kama ambavyo barua za zuio kutoka halmashauri walizopewa zinavyoeleza.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.