Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Reuben Sixbert Jichabu amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewasikia na kuwafikia wananchi wa Mji Masasi kwa kutoa jumla ya shilingi 13,847,872,949 kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo, Utalii, Viwanda na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa waandishi wa habari na ofisi ya Idara ya Habari maelezo katika mkutano uliofanyika Desemba 19, 2023 katika ukumbi wa BOT Mtwara.
Kwa upande wa elimu, amesema jumla ya fedha sh. 3,679,203,376 zimepokelewa na kutekeleza miradi mbalimbali ya shule.
Aidha amesema Halmashauri imepokea jumla ya fedha sh. 682,300,000 kutoka Mradi wa boost kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya shule za Msingi.
Amesema jumla ya fedha sh. 120,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya kujenga vyumba 2 vya madarasa na bweni katika shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Masasi.
Amesema jumla ya fedha sh. 621,750,000 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ukamilishaji wa maboma 8 sh. 93,750,000, ujenzi wa uzio shule ya watoto wenye mahitaji maalum sh 30,000,000.
Aidha amesema Serikali imewezesha Ujenzi wa vyumba vya madarasa 18 yenye thamani ya sh. 388,000,000 katika shule ya msingi ya Migongo na Mkomindo pamoja na sh. 110,000,000 za ujenzi wa nyumba 4 za walimu. Ruzuku ya uendeshaji wa elimu bila malipo katika kipindi cha awamu ya 6 ni sh. 2,175,328,376.
Amesema Jumla ya sh. 79,825,000 Zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa ya awali ya mfano iliyojengwa katika shule ya msingi ya Nyasa na ukarabati wa kituo cha walimu Mkomaindo sh. 22,000,000.
Aidha amesema Jumla ya fedha sh. 3,457,052,827 zimepokelewa na kutekeleza miradi mbalimbali ya shule.
Halmashauri imepokea jumla ya fedha sh. 1,030,552,827. Kwa ajili ya kujenga shule mpya mbili ya sekondari ya Temeke na Jida.
Jumla ya fedha sh 54,400,000 zimepokelewa kwa jili ya kujenga vyumba 2 vya madarasa na matundu ya vyoo 4 katika shule ya sekondari ya wasichana Masasi.
Jumla ya fedha sh. 700,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya kujenga vyumba 35 vya madarasa katika sekondari ya Masasi kutwa(3) Nangaya (4) Anna abdala (4) Mtandi (5) sululu(3) Mtapika (4) Masasi wasichana (4) Marika (4) chanikanguo (4)
Jumla ya fedha sh. 25,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya kukamilisha vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari ya Mtandi.
Jumla ya fedha sh. 1,254,300,000 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambapo amesema Kati ya hizo sh. 366,400,000 zimetumika kujenga vyumba 17 vya madarasa na matundu 24 ya vyoo katika shule 6 , ujenzi wa miundo mbinu shule kongwe ya Masasi wasichana sh. 387,900,000, na ujenzi wa madarasa 5 na bwalo ya kidato cha tano katika shule ya sekondari Mtapika sh. 320,000,000, pamoja na sh. 180,000,000 za ukamilishaji wa maabara katika sekondari ya Masasi Kutwa, Anna abdalah na Chanikanguo.
Sambamba na hilo amesema Sekta ya afya imeendelea kutekelezwa kwa vitendo ambapo jumla ya fedha sh 2,615,000,029 zimepokelewa na kutekeleza miradi mbalimbali katika vituo vya kutolea huduma ya afya.
Amesema Jumla ya fedha sh. 300,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya kujenga Jengo la kutolea huduma za dharura(emergency) katika Hospitali ya Mkomaindo. Jumla ya fedha sh. 500,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Mtandi
Aidha Jumla ya fedha sh. 115,000,029 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi(3 kwa1 ) zahanati ya Namatunu sh. 95,000,000 pamoja na ukarabati wa wodi ya wagonjwa wanaotengwa hospitali ya Mkomaindo sh. 25,000,029.04.
Jumla ya fedha sh. 1,700,000,000.00 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya. Kati ya hizo sh. 900,000,000 ni kwa ajili ya Ukarabati wa Hospitali ya Mkomaindo, sh. 200,000,000 ni za ujenzi wa zahanati za matawale na Napupa pamoja na sh. 600,000,000 za ununuzi wa vifa tiba katika vituo vya afya 2 na zahanati 3
Jumla ya fedha sh. 150,000,000.00 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi wa mji Masasi.
Halmashauri ya Mji Masasi katika kipindi cha uongozi cha awamu ya sita (6) imefanikisha kuongeza idadi ya vikundi vilivyosajiliwa kutoka vikundi 75 mwaka 2020/21 hadi 118 kufikia Dec 2023. Vikiwemo vikundi nvya wanawake 68, vijana 44 na wenye ulemavu vikundi 6.
Kiasi kilichokopeshwa katika kipindi cha awamu ya sita (6) ni sh. 661,350,326 ambapo wanawake wamekopeshwa sh. 398,050,326.00 vijana wamekopeshwa sh. 237,300,000 na wenye ulemavu wamekopeshwa sh. 26,000,000.00
Katika kipindi cha awamu ya 6, Halmashauri imepokea fedha za kutekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini pamoja na utoaji wa ajira kwa walengwa TASAF sh. 3,797,994,709.
Amesema viongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe, Geoffrey Mwambe wataendelea kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unawanufaisha wananchi wa Masasi Mji.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.