Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbasi ameukabidhi Rasmi Mwenge wa Uhuru apirl 11,2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Taleck.
Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa eneo la Nyangao Mkoani humo ,Halmashauri ya Mji wa Mtama.
Ukiwa Mkoa wa Mtwara Mwenge wa uhuru umetembea umbali Zaidi ya kilometa 948 na kukagua Miradi 54 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 31.
Aidha Mwenge wa Uhuru umekagua na kutembelea miradi yote na kuridhia kuweka mawe ya msingi kwa kuwa imekidhi vigezo vyake.
Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg Abdallah Shaibu Kaim ameupongeza Mkoa wa Mtwara kwa kuwa na Miradi yenye viwango na kuomba kuendelea kumsaidia mh; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia Majukumu yao ya ujenzi wa Taifa.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.