Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala ameipongeza Halmashauri ya Mji Masasi kwa kupata hati safi katika taarifa ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Kanali Sawala amesema hayo Julai 01, 2024 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 2022/2023.
“Nawapongeza sana kwa kupata hati safi, maana yake kuna watu wamefanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na miongozo lakini pia nakupongeza Mhe. Mwenyekiti Mhe. Hashim Namtumba na Baraza lako la Waheshimiwa Madiwani kwa usimamizi mzuri wa Halmashauri lakini pia Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu kwa utekelezaji wa maagizo ya mbalimbali” Amesema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Hashim Namtumba amesema upatikanaji wa maendeleo unafanikiwa kutokana na ushirikiano bora baina ya waheshimiwa Madiwani na Watendaji.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Lauteri John Kanoni amesema hati safi ndio kipimo cha utendaji na kuwapongeza waheshimiwa madiwani kwa kusimamia utendaji wa halmashauri uliosababisha kupatikana kwa hati safi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.