Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapa tabasamu watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Masasi iliyopo Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara kwa kutoa vifaa vya kuwasaidia na zawadi mbalimbali.
Akikabidhi Vifaa na Zawadi hizo agosti 13, 2023 kwa Uongozi wa shule ya Msingi Masasi, kwa niaba ya Rais, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi. Erica Yegella amesema Rais ameendelea kuwajali na kuwapa tabasamu watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuhakikisha wanapata fursa bora ya elimu, mazingira bora, huduma bora za kijamii, upendo, amani na kila jema lenye kuchochea maendeleo ya watoto wenye mahitaji maalumu katika jamii.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi nyingi na muhimu zitakazowasaidia wenye mahitaji maalumu kwa muda mrefu.
“Nakabidhi zawadi mbalimbali kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan zikiwemo, White cane, Braille paper carton, Audible football/bell ball ,Universal braille kit, Braille slates with stylus, Perkins braille machines, Hand magnifies, Low vision stand, Albino special lotion tube, Albino special hat, Albino sunglasses, Puzzles, Rattles, Plastic building blocks, Push animal toys, Wallcharts animals, Wallchart alphabet, Wall chart numbers, Flash cards, Skipping ropes, Square wooden blocks, na Porcupine ball” Mkurugenzi
Aidha amesema binafsi anaunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia kwa kutoa bima za afya kwa watoto wote wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo.
“ Mhe. Rais wetu ameshaleta vifaa vya kutosha hapa, na mimi binafsi namuunga mkono mheshimiwa Rais kwa kutoa bima za afya kwa watoto wote hawa, zoezi hili linaanza mara moja kwa watoto hawa kupigwa picha na kulipia bima zao, kwa sababu kuna magonjwa mbalimbali ni muhimu tulinde afya zao, bima hiyo nitaitoa mimi ” Mkurugenzi Bi. Erica Yegella.
Amewakaribisha wananchi wa Masasi na wa maeneo mbalimbali kuendelea kutoa msaada wa vifaa na zawadi mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo.
Katika hatua nyingine, Wadau mbalimbali na watumishi wameunga mkono juhudi hizo kwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo chakula kama unga, mchele, sukari, maharage, mafuta, sabuni, vinywaji na zawadi mbalimbali.
Awali akisoma taarifa ya Shule hiyo, Mkuu wa shule amesema shule ya Msingi Masasi ni shule ya Msingi Jumuishi iliyoanzishwa mwaka 1954 ikiwa na jumla ya wanafunzi 626 ambapo wavulana ni 318 na wasichana 308.
Amesema kati yao wenye mahitaji maalumu ni 65 ambapo wavulana ni 35 na wasichana 30 wakiwa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni wasioona wakiwa 30, wenye ulemavu wa ngozi ( albinism) 26, na walemavu wa viungo 8.
Amesema zawadi hizo zitawasaidia sana katika kuboresha afya zao na maendeleo yao kielimu kwa ujumla.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.