Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amefurahishwa na kuipongeza Hospitali ya Halmashauri ya Mji Masasi ya Mkomaindo kwa ubora na weledi wa watalaamu wa Afya katika utoaji wa huduma za Afya.
Ametoa pongezi hizo leo Julai 11, 2024 katika ziara ya kutathmini na kukagua ubora wa utoaji wa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya wanayoendelea kuifanya katika Mikoa yote Nchini.
“ Lengo la ziara yetu ni kuangalia Je uwekezaji ambao Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameufanya kama unaendana na huduma ambazo wananchi wanazipata kwa viwango vilivyowekwa na Wizara ya Afya au kimataifa kama Shirika la Afya Duniani. Tunatembelea mikoa yote, leo tumeingia katika mkoa wa 22, Mtwara na hapa tupo katika Hospital ya Halmashauri ya Mji Masasi, Hospitali ya Mkomaindo, tunatazama uwekezaji huu mkubwa kama unaleta matokea tarajiwa hasahasa EMD na ICU, Hapa Hospitali ya Mji Masasi Mkomaindo niseme tu tumekuwa na furaha sana kama TAMISEMI, tumeona kwa vitendo, watumishi wamepata mafunzo na wanayatumia kwa ufasaha sana, nilivyowatathmini hata tukisema twende hospitali za Rufaa, watumishi wa Mkomaindo mtatumia hizi mashine kwa ufasaha sana ngazi za rufaa, hongereni sana.” Amesema.
Katika zoezi za kukagua na kufanya tathimini Mkurugenzi huyo, ameongoza zoezi la kupima kwa vitendo ufasaha wa watalaamu wa Afya katika kutumia vifaa na kuhudumia wagonjwa wa dharula, huku akiahidi kuwatumia watumishi wa Mkomaindo kuwajengea uwezo watumishi wa maeneo mengine ndani ya Mkoa na Nchini.
“Tumefanya kwa vitendo kwa mimi kuwa mgonjwa, mmeeleza vizuri kwa kuzingatia standard zote, tumevutiwa sana na tunaamini huu uwekezaji unaofanyika ulete matokea chanya kama Hospitali ya Mkomaindo, Hospitali ya Masasi unavyofanya kazi, Hongereni sana, mganga mfawidhi, Mganga Mkuu wa Halmashauri na Mganga Mkuu wa Mkoa”.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.