Mkuu wa Wilaya ya Masasi Claudia Kita tarehe 8,12,2022 amekabidhi Reflector 500 na kofia ngumu (Helmet) 30 kwa waendesha Bodaboda wilayani huo msaada uliotolewa na Ofisi ya kuu wa Mkoa wa Mtwara na kampuni ya maji ya Watercom ya jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo DC Kita amewataka waendesha Bodaboda hao kutumia vitendea kizi hivyo wakati wote wanapokuwa barabarani kwani ni msaada mkubwa kwao kutambulika na vyombo vyingine vya moto kama magari makubwa lakini pia kuwakinga na majeraha pindi inapotokea ajali.
Amesema pia kuna vitendo vingi vya kiuhalifu ambavyo huhusisha Bodaboda na kutambulika inakuwa vigumu lakini vifaa hivyo sasa vitasaidia kutambua kwani kila aliyekabidhiwa ametambuliwa kwa viambata vyake na pia kupewa namba maalum.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Wilaya ya Masasi Arif Abdalah ambaye pia ni mwakilishi wa Watercom kanda ya kusini amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza ajali kwani wamewapatia vijana hao elimu ya kutosha ya namna ya kujikinga na kuwakinga wengine na ajali wawapo barabarani na kuahidi kusaidia vijana wa maeneo mengine ya Mtwara wakianzia na Masasi.
Nao wandesha Bodaboda hao wameishukuru serikali na kumuahidi Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa wataitumua elimu waliyopata pamoja na kuwa mabalozi kwa wengine
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.