Mganga Mkuu halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Dr Salum Gembe amewaomba kamati ya kushughulikia majanga ya dharula halmashauri ya Mji Masasi kujitoa kwa Jamii kwenda kutoa Elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola .
Ameyasema hayo agost 30,2022 katika kikao cha kwanza cha maandalizi ya kujikinga na Ugonjwa wa Ebola ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji ambacho kilihudhuriwa na wataalamu wa Afya ,Madereva wa magari ya vituo vya afya ,ustawi wa jamii pamoja na Idara ya Maendeleo ya jamii.
Dr Gembe amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwaandaa wataalamu kisaikolijia kuhusu ugonjwa wa Ebola lakini pia kutaka kufahamu dalili ,namna ya kujikinga na jinsi ya kusimamia kambi la watu wenye maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola na kutenga maeneo maalum ambayo mgonjwa akitokea ili aweze kuhifadhiwa.
Afisa afya Halmashauri ya Mji Masasi Benjamin Eliasi ambae pia ni muwasilishaji wa mada kuhusu Ugonjwa wa EBOLA ametoa Elimu kwa washiriki wa kikao hiko kuhusu dalili za Ugonjwa huo,namna ya kujikinga na namna ya kumtambua Mtu mwenye maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola .
“Ugonjwa wa Ebola ulianza mwaka 1976 Nchi ya Congo DrC na baadae ulisambaa katika Nchi za Sudan ,Afrika ya kati ,Uganda na Nchi za Ulaya na hadi sasa kwa Tanzania hatujapata kesi yoyote kuhusu Ugonjwa wa Ebola.”Benjamin Elias
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.