.Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Eliasi Ntiruhungwa Ametoa Agizo kwa Maafisa Watendaji Kata kwenda kuwahamasisha Wazazi/Walezi kuhusu Uchangiaji wa Chakula Mashuleni Kwa Shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo halmashauri ya Mji Ili kuongeza Lishe Bora Kwa watoto.
Agizo Hilo amelitoa Leo November 18 katika Kikao Cha Tathimini ya Lishe Kwa Robo ya kwanza 2022/20223 ,kikao ambacho kilihudhuriwa na wadau Mbalimbali wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi ,Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Watendaji kata, Mwakilishi kutoka kituo Cha Radio Fadhila na Mwakilishi kutoka Bwakwata.
Aidha Ntiruhungwa ameeleza kuwa Wataalam wamefanya Tafiti na kubaini maadhara ya kutopata lishe Bora na Mkoa wa Mtwara upo katika mikoa ambayo inaongoza Kwa Udumavu ndiyo Maana Matokeo ya Elimu yanashuka kutokana na Ukosefu wa Lishe Bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta amewataka Maafisa Watendaji Kata kwenda kutekeleza Yale waliyoelekezwa kwa kufuata kanuni na utaratibu wa Lishe Bora na ana Imani Maelekezo yote yaliyotolewa yataenda kufanyiwa Kazi.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.