Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua Miradi mitatu (3) na kuweka Mawe ya Msingi katika Miradi miwili (2) na kukagua na kuona Miradi miwili (2) Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimepokelewa leo Juni 6, 2024 katika eneo la Viwanja vya Mlundelunde kata ya Mumbaka kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge amezindua Mradi wa Maji Namatunu, amezindua Karakana ya Utengenezaji wa Magari, amezindua Ujenzi wa Jengo la Upasuaji Hospitali ya Mkomaindo, ameweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Vyumba tisa vya madarasa shule Kongwe ya msingi Mkomaindo na Ujenzi wa Barabara ya Top Queen Nyasa Magengeni kiwango cha Lami yenye urefu wa Km 0.7 sambamba na kukagua na kuona shughuli za ujasiriamali za vijana wanaotengeneza vifaa vya aluminium na kukagua shamba la miti TFS lenye Ukubwa wa ekari 94.57
Mwenge wa uhuru ukiwa Halmashauri ya Mji Masasi umekimbizwa Umbali wa km 66.3, na kupita katika katika Tarafa moja, kata kumi, vijiji tisa, na mitaa kumi na sita.
Mwenge wa Uhuru umepitia, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi yote saba ya Halmashauri ya Mji Masasi yenye gharama ya bilioni 3.2.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 ni, “TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU”.
MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.