Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Masasi Mjini Ndg. Prosper R. Luambano amemtangaza DKT. LEONARD DOUGLAS AKWILAPO kutoka CCM kuwa mshindi wa kiti wa Ubunge Jimbo la Masasi Mjini baada ya kupata jumla ya kura 58615.

Aidha ametangaza matokea ya kura ya wagombea Ubunge Jimbo la Masasi Mjini kama ifuatavyo;
Ahmadi Musa Nannyoho Kutoka N.L.D amepata jumla ya kura 216.
Salum Ahuni Mwinyikheri kutoka CUF amepata jumla ya kura 982.
Zawadi Mustafa Nayopa kutoka AAFP amepata jumla ya kura 313.
Maimuna Hafidhi Maliki kutoka ACT-Wazalendo amepata jumla ya kura 681.
Na Steward Ernest Kaking kutoka CHAUMMA amepata jumla ya kura 978.

Amesema shughuli za Uchanguzi Jimbo la Masasi Mjini zimefanyika kwa utulivu na amani pasipo kukutana na changamoto yoyote kubwa kutoka na ushirikiano bora kutoka vyama vya siasa, muitikio wa wananchi na wadau mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.