Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara Elias Ntiruhungwa Ametia Saini Mkataba wa Usimamizi wa utekelezaji wa Afua za Lishe unaotarajiwa kutekelezwa Halmashauri ya Mji Kwa Mwaka 2022/2023.
Mkataba huo Umesainiwa November 18,2022 baina ya Mkurugenzi , Maafisa Watendaji kata wote wa Halmashauri ya Mji Masasi , Afisa Utumishi pamoja na Wakuu wa Idara.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi amesema kuwa kila Mtendaji na kata yake aende akasimamie Shughuli za Lishe Kama makubaliano yaliyopo kwenye Mkataba wake ambao ameusaini Kwa sababu Suala la Lishe ni kubwa Kwa Maendeeleo ya jamii zetu na Taifa Kwa ujumla.
MASASI TOWN COUNCIL
Anuani ya Posta: P.O BOX 447 MASASI
Simu Ya Mezani: +255 23 2510685
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: info@masasitc.go.tz
Haki Miliki@ Halmashauri ya Mji Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa.